Jaji Magimbi kusikiliza rufaa ya Godbless Lema Desemba 28
REMA |
JAJI
Salma Magimbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ndiye atakayesikiliza
rufaa ya kutaka dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema,
Desemba 28 mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Wakili wa Lema, Sheck Mfinanga alisema
rufaa hiyo namba 126 ya mwaka 2016, imepangiwa kusikilizwa na Jaji huyo.
Alisema kimsingi wanalalamikia uamuzi wa Mahakama kutomwachia huru,
licha ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumpatia dhamana.
Awali,
uamuzi uliotolewa Novemba 11 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha na Hakimu Desderi Kamugisha, ambapo Lema anakabiliwa na kesi
namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, uliweka wazi
dhamana.
Hakimu
Kamugisha alikubali kutoa dhamana kwa madai kuwa sheria haizuii kumpa
dhamana mtu kwa kesi ya uchochezi, ila kabla ya kutoa masharti ya
dhamana licha ya kutamka dhamana ipo wazi, mawakili wa serikali
walipinga kumpatia dhamana Lema, kwa madai wameonesha nia ya kukata
rufaa.
Kutokana na mawakili hao kusema hivyo, Hakimu aliamua kesi hiyo ibaki kama ilivyo na mtuhumiwa asubiri maamuzi ya Mahakama Kuu.
Lema
alilazimika kwenda mahabusu hadi sasa katika Gereza Kuu la Kisongo.
Baada ya hatua hiyo, mawakili wa Lema wakiongozwa na Sheck Mfinanga,
walianza kutafuta suluhisho la mteja wao kupata dhamana na walianza na
kuandika maombi na kuitaka Mahakama Kuu kufanya marejeo kwa kuitisha
faili la kesi hiyo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Lakini,
ombi lilitupwa na Kaimu Jaji Mfawidhi, Sekela Moshi, Novemba 11 mwaka
huu kwa madai kuwa walikosea, badala ya kufanya marejeo walitakiwa
kukata rufaa. Mawakili hao walilazimika kukata rufaa siku hiyo hiyo na
Desemba 2 mwaka huu, ilitupwa na Jaji Fatuma Masengi kwa madai kuwa
ilikuwa nje ya muda.
Baada
ya hatua hiyo, mawakili hao walipeleka ombi Mahakama Kuu, kuomba
kuongezewa muda wa kupeleka notisi ya kukata rufaa yao juu ya dhamana na
hatimaye Desemba 20, Jaji Dk Modesta Opiyo, alikubali na kumwongezea
muda Lema wa siku 10.
Siku
hiyo ya kuongezewa muda, mawakili wa Lema walifanikiwa kukata rufaa
hiyo. Lema anashikiliwa kwa zaidi ya mwezi katika mahabusu ya Gereza Kuu
Kisongo.
Alikamatwa
Novemba 2 mwaka huu nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na
alifikishwa mahakamani Novemba nane mwaka huu, akikabiliwa na mashitaka
ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.HABARINA MPEKUZIHURU
No comments