Diva acharuka vikali baada ya kuhusishwa na Team Kiba
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva amewacharukia vikali wale wanaodai yeye ni Team Kiba baada ya kufanya interview ya mchekeshaji Mama Ashura ambaye alitumia muda mwingi kuukosoa mwenendo wa Alikiba katika muziki kwa sasa.
Diva amesema yeye hana team na anaheshimu kazi yake na watu wanapaswa kuelewa kuwa kwa sasa yupo buys sana hawezi kushughulika na mambo kama hayo.
“Nimepata malalamiko baadhi ya watu Oh kwanini umemualika Mama Ashura, wewe si team Kiba Oh Diva this and that. Naomba ni make it very clear mimi sina U team, mambo ya Uteam yanagawa mashabiki wangu, sitaki kwanza hata kusikia mambo hayo tena, Im over that Path. Mungu mwenyewe anajua nilivyo busy saa hii building my life and my future jaman , have alot in my plate sahan yangu imejaa sana.
“Huo muda tena sina tena and love everybody yes napenda kila mtu ata haters sababu wananifanya niwe famous, yes ila sichagui sibagui ataenizika simjui wanasema waswahili, Mi nahudumia watu wote sihudumii pande moja tu, Sitaki Gawa shabiki zangu sababu ya vitu ambavyo havinipi faida maishani, tuendeleen kuwa marafiki tuheshimiane,” ameandika Diva Instagram na kuongeza.
“Hivyo basi namualika yeyote kwenye show yangu nikijisikia na watu wakimuhitaji, sina pande yoyote ile niko busy nafanya kazi yangu na naiheshimu sana kama ninavyoiheshimu serikali, nawapenda sana ila being professional kumenipenda zaidi, I choose to be happy and means i’ll support good music regardless, na ukinikosea I m free shot you with Nothing but the truth, I m free soul, peace out!!,” amesisitiza.
No comments