Usikose Hizi Hapa

Tetesi za soka Ulaya leo Jumamosi 02-09-2017

Real Madrid ilikubali uhamisho wa winga Gareth Bale kuelekea Manchester United lakini mchezaji huyu akakataa uhamisho huo.(Don Balon, via Daily Star)
Real Madrid ilikubali uhamisho wa winga Gareth Bale kuelekea Manchester United lakini mchezaji huyu akakataa uhamisho huo.(Don Balon, via Daily Star)
Ombi la Liverpool kutaka kumsajili mchezaji wa Monaco Thomas Lemar limekataliwa na klabu hiyo lakini bado tmu hiyo inaweza kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 mnamo mwezi Januari(L'Equipe via Daily Express)
Wachezaji wenza wa Brazil wa kiungo wa kati wa Liverpool Philipe Coutinho mwenye umri wa miaka 25 walimuona mchezaji huyo akilia kabla ya mechi ya kufuzu kwa kombe la duniani dhidi ya Ecuador baada ya ombi lake la kutaka kuhamia Barcelona kukataliwa. (Calcio Mercato - Spanish)
Manchester City wanatarajiwa kuwasilisha malalamishi rasmi dhidi ya Arsenal baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez
Manchester City wanatarajiwa kuwasilisha malalamishi rasmi dhidi ya Arsenal baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Sun)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Paul Merson amesema kuwa kilabu yake ya zamani ilikosea kwa kutomuuza Sanchez kwa kuwa wanahitaji fedha kununua walinzi. (Sky Sports)
Na Manchester City inajiandaa kuwasilisha ombi jingine la kitita cha chini kumsajili mshambuliaji huyo wa Chile mnamo mwezi Januari.(Sky Sports)
David Beckham huenda akaomba kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, wakati atakapoanzisha timu yake katika ligi ya Major League mjini Miami (mirror)
David Beckham huenda akaomba kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, wakati atakapoanzisha timu yake katika ligi ya Major League mjini Miami (mirror)
Chelsea ilifeli kuwasajili wachezaji watatu waliohitajiwa na mkufunzi Antonio Conte , Romelu Lukaku, Alex Sandro na Virgil van Dijk, lakini klabu hiyo inaamini raia huyo wa Italy ana kikosi chenye uwezo wa kugombea taji la ligi ya Uingereza na lile la vilabu bingwa.(Daily Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ameshirikishwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa ligi ya Premia licha ya ripoti kwamba hatorudi kuichezea Chelsea msimu huu.(Mirror)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, ameshirikishwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa ligi ya Premia licha ya ripoti kwamba hatorudi kuichezea Chelsea msimu huu.(Mirror)
Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard, 26, amesema kuwa huenda ana thamani ya 300m euros (£265m) katika soko la uhamisho la msimu huu kufuatia kununuliwa kwa Neymar aliyegharimu £200m (Daily Mail)
Tottenham na Chelsea itatumai kumsajili kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley mnamo mwezi Januari
Tottenham na Chelsea itatumai kumsajili kiungo wa kati wa Everton Ross Barkley mnamo mwezi Januari wakati ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23-atagharimu chini ya £35m zilizokubaliwa na Blues msimu huu. (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez, yuko tayari kuchukua ukufunzi wa West Ham iwapo Slaven Bilic ataondoka kufuatia kushindwa kufanya usajili msimu huu (Guardian)

No comments