MAKOCHA WA SOKA TANZANIA BARA KUKUTANA FEBRUARI 18,UCHAGUZI KAMATI YA UTENDAJI KUTANGAZWA
Mkutano Mkuu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) Mkoa wa kisoka wa Kinondoni utafanyika Februari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam katika ukumbi utakaotangazwa baadaye.
Mbali ya ajenda za kawaida za kikatiba, Mkutano huo utaoongozwa na Mwenyekiti wake Eliutery Mholery utapanga tarehe ya uchaguzi ya Kamati mpya ya Utendaji baada ya iliyopo kumaliza muda wake.
Pia Mkutano huo utazungumzia uanzishaji wa Chama cha Makocha cha Wilaya mpya ya Ubungo ambayo imemegwa kutoka Wilaya ya Kinondoni.
Tayari Wilaya ya Ubungo imeshasajili na kufanya uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ubungo (UFA).
Tunatoa mwito kwa makocha wote wa TAFCA Kinondoni kuhudhuria Mkutano huo muhimu kwa ustawi wao pamoja na mpira wa miguu kwa wilaya za Kinondoni na Ubungo.
Boniface Wambura MGOYO
Mjumbe Kamati ya Utendaji TAFCA Kinondoni
No comments