Huyu ndio staa wa filamu wa kike aliyelipwa zaidi 2017
Muigizaji kutoka Hollywood Emma Stone ametajwa kuongoza orodha ya mastaa wa filamu wa kike ambao wamevuta mkwanja mrefu zaidi mwaka huu.
Mrembo huyo ambaye ana umri wa miaka 28, ametajwa kulipwa kiasi cha dola milioni 26 kuanzia Juni 2016 mpaka kufikia Juni 2017.
Emma ametokea katika filamu kibao ikiwemo ‘The Amazing Spider Man’, ‘Zombie Land’, ‘Friends With Benefit’ na nyingine.
Naye Jennifer Lawrence ambaye aliongoza orodha hiyo kwa mwaka uliopita anashika nafasi ya tatu kwa sasa ambapo ametajwa kulipwa kiasi cha dola milioni 24 kwa mwaka huu.
No comments