Baraka The Prince aanika kile alichokiona ndani ya RockStar4000
Msanii Baraka The Prince amedai moja ya sababu ya yeye kuachana na label yake ya zamani ya RockStar4000 ni usimamizi mbovu juu yake.
Muimbaji huyo amedai takwimu zake zimezidi kushuka katika kazi zake alizokuwa anasimamiwa na uongozi huu pamoja na kutolewa nyimbo moja kwa mwaka tofauti na yeye alivyokuwa anategemea atafanya.
“Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu hii ndiyo kazi yangu na mwisho wa siku hii mimi ndiyo kila kitu na sina kazi nyingine, kwa hiyo nikiona kuna vitu havipo ‘serious’ na havipo ‘sure’ kwa upande wa watu ninaofanya nao kazi sina budi kujiengua na kufanya mwenyewe. Nipo sawa na hakuna mtu ambaye anaweza kuniingilia juu ya hilo mwisho wa siku mimi ndiyo ninajua kazi ninayofanya na ugumu wake katika kujenga ‘brand’ yangu, najua ugumu wa kila kitu ‘so’ haya ni maamuzi yangu”, Baraka aliiambia Enewz ya EATV.
Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kusema “mimi ndiyo mwenye kauli ya mwisho. Sitaki kuongelea masuala ya mikataba kwa sababu kipindi nina saini tokea awali sikuweza izungumzia wakati naingia kwa hiyo sitasema lolote juu ya hilo kwa sasa”,amesisitiza Baraka.
Kwa upande mwingine, Baraka amesema yeye hafanyi muziki kwa ajili ya menejementi bali anafanya muziki kwa mashabiki wanamuwezesha kumlipa katika nyimbo zake wanazozipakua katika mitandao.
No comments