Usikose Hizi Hapa

Matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne Yatangazwa....... St. Franscis, Kilimanjaro Islamic na Kaizerege Zaongoza



Baraza la Mitihani nchini – NECTA limetoa matokeo ya mitihani ya upimaji kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa shule zote za msingi nchini pamoja na ule wa kidato cha pili kwa wanafunzi wa shule za sekondari yanayoonesha ufaulu kuongezeka kwa 1.9%.

Katibu Mtendaji wa Baraza lza Mitihani nchini Dkt Charles Msonde ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo katika hali isiyo ya kawaida, shule tisa kati ya kumi zilizofanya vibaya katika mtihani wa kidato cha pili nchini, zimetoka mkoani Mtwara kama zinavyoonekana hapa

Amesema ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.9 kutoka 89.12% mwaka 2015 hadi kufikia 91.02% mwaka 2016 ambapo wanafunzi 372,228 wamepata alama zinazowawezesha kuingia kidato cha tatu huku wanafunzi 36,737 wakishindwa kufikisha alama hizo.

Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika shule 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya I, II, na III ni 178,115 sawa na asilimia 43.55

Kuhusu ufaulu wa masomo, amesema, katika masomo ya Civics, History, Geography, Kiswahili, Phiysics, Chemistry, Chemistry, Biology na Basic Mathematics umepanda ikilinganishwa na mwaka 2015.

Aidha ufaulu kwa somo la English Language pekee ndio ambao umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2015.

Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 90.06 ya wanafunzi wote, wamefaulu na soko lenye ufaulu wa chini zaidi ni Basic Mathematics ambapo asilimia 21.55 wamefaulu.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi ni Teckla Erasmo Haule kutoka Canosa ya Dar es Salaam akifuatiwa na Joseph Fabian Kalabwe wa Kwema Modern ya Shinyanga na Mirable Rayner Matowo wa Canosa ya Dar es Salaam.

Katika wanafunzi 10 bora kitaifa, wanafunzi 9 ni wasichana, na watano kati yao wanatoka Feza Girls.

Matokeo ya wanafunzi 31 yamefutwa baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu.







No comments