Timbulo: 'Usisahau' ingebuma nisingefanya muziki Tena
Msanii wa kizazi kipya, Ally Timbulo ambaye kwa muda mrefu hajaonekana kwenye fani, hivi karibuni baada ya kutoa kibao chake kipya, alifunguka kwa kutaja mambo ambayo angefanya endapo kichupa chake kipya kisingefanya vizuri sokoni.
Amefunguka kuwa kama wimbo wake mpya ‘Usisahau’ aliomshirikisha baraka the Prince usingefanya vizuri ingekuwa sababu ya yeye kuachana na muziki na kufanya kilimo kama ajira yake.
Akizungumza katika kipindi cha Dj Show Radio one, Timbulo, alisema kuwa waliwekeza zaidi kwenye wimbo huo na ulikuwa ukitegemewa na menejimenti yake pamoja na yeye mwenyewe kufanya vizuri kabla haujatoka.
”Kwa jinsi nilivyokuwa ‘nimeinvest’ kwenye hii ngoma na jinsi tulivyokuwa tunaitegemea na menejiment, pengine tungekuwa tunaongelea vitu vingine kama ngoma isingefanya poa, kwa kuwa ‘investment’ yake ilikuwa kubwa sana, pengine ingekuwa sababu ya mimi kutokuwepo tena kwenye muziki ambao naendelea kuufanya” alisema Timbulo.
Timbulo alisema kuna uwezekano mkubwa angerudi darasani au hata shamba kulima, kama wimbo huo usingeenda na matarajio yake.
Baadhi ya nyimbo ambazo amewahi kufanya Timbulo ni pamoja na Sina makosa, Samson Delila na Niende zangu’.
No comments