Usikose Hizi Hapa

G-Nako: Waongozaji wengi wa Kibongo wanashindwa ‘kudeliver’ video namna tunavyotarajia ziwe

www.planetmwamba.blogspot.com
Rapper G-Nako amedai kuwa kasoro kubwa waliyonayo waongozaji wengi wa video za muziki wa Tanzania ni kukabidhi video zilizo chini ya kiwango au nje ya matarajio ya msanii.


Akiongea kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir kilichoruka jana EATV, rapper huyo amesema hiyo ni sababu wasanii wenye uwezo huenda kufanya video zao Afrika Kusini.
“Unaweza ukawa umempa kila kitu, labda anataka sijui gari aina fulani sawa linapatikana, model mzuri anapatikana, lakini inapokuja sasa wakati wa kuedit na kupewa kazi kwa jicho lako ulivyokuwa unategemea haiwi vile ulivyokuwa unategemea,” amesema.
“Sisi sio wataalam sana wa kukiangalia kitu kwa undani kama ambavyo mtu mwingine anajua kama director ama kama mtu mwingine anayejua kuedit lakini ukikiangalia kitu unajua hiki ni kizuri, ama ni kibaya.”
G-Nako amedai kuwa ni tofauti kwa waongozaji wa nje ambao huweza kukupa kila kitu ambacho ulikuwa umekijengea picha hata kabla video haijatoka.

No comments