Usikose Hizi Hapa

Huzuni Yatawala Mahakamani Wakati Daktari Akitoa Ushahidi Dhidi ya Scorpion

Daktari  Bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Christine Mataka ambaye alimpokea na kumhudumia, Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho na Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa shahidi wanne katika kesi hiyo upande wa serikali, ametoa siri nzito ya tukio hilo.

Dokta Mataka amesema alikuwa daktari wa kawaida kwa muda mrefu lakini alitunukiwa digrii ya pili (Master’s) na kuwa daktari bingwa wa matatizo ya macho miaka 14 iliyopita.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga bingwa huyo alisema macho ya Said hayakutobolewa kama inavyosemwa na watu kwenye vyombo vya habari isipokuwa yamenyofolewa na kuondolewa kabisa.

Majeruhi alifika hospitali macho yake yakiwa yamenyofolewa na kubaki hukohuko,hospitali hakufika hata na mabaki ya goroli.

Akielezea kitaalamu Dokta Mataka alisema kwa kawaida mtu anapotobolewa macho na kitu chochote ni lazima ukute goroli zikiwa zimepasuka na utete wenye utelezi unakuwa umetapakaa machoni lakini kwa majeruhi huyo goroli za macho yote mawili zilikuwa hazipo kabisa.

"Ukweli hiyo hali ilinishangaza sana kwa miaka 14 nikiwa kama daktari bingwa wa macho sijawahi kukutana na tukio kama hilo hivyo baada ya kupigwa na butwaa niliwapigia mabingwa wenzangu waje kujionea hali hiyo na tushauriane jinsi ya kufanya.

"Hata wao walivyofika wote walishangaa na kuniambia nao hawajawahi kukutana na hali hiyo.

"Nilimtibia majeruhi wakati huo huo nilikuwa nikimuongelesha na kumuuliza yaliyomsibu ambapo aliniambia wakati akinunua kuku pale Buguruni ndiyo akatokea mtu na kuanza kumshambulia.

"Nikamuuliza kama anamfahamu hiyo mtu aliniambia akimuona atamtambua.


"Baada ya matibabu nilimpeleka wodini na kumuandikia tarehe za kuhudhuria kliniki na nilimuambia kuwa katika maisha yake hawezi kuona tena hivyo ajifunze kuishi maisha ya mtu asiye na macho.

"Baadae alipoanza kuja kliniki aliniambia kuwa mama yake alikuwa akitaka kumpa jicho lake moja lakini nilimueleza ukweli kuwa hilo haliwezekani.

"Huwezi kulihamisha jicho halafu likawa hai hiyo huduma haipo hapa duniani.

Baada ya kutoa ushahidi wake mbele ha Hakimu Frola Haule kesi hiyo iliahirishwa mpaka Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo ambapo daktari bingwa wa tumbo ambaye nae alimtibu majeruhi huyo anatarajiwa kutoa ushahidi wake kwa upande wa serikali.

No comments