Lady Jaydee aonjesha ujio wa album mpya ‘Woman’
Kupitia Instagram, Jide ameshare kile kinachoweza kuwa ndiyo cover rasmi la album hiyo. Muimbaji huyo mkongwe pia anatarajia kufanya concert kubwa kwaajili ya uzinduzi wa album hiyo.
“Natarajia kufanya concert kubwa kwaajili ya launch ya album ya Woman ambayo itakuwa ni mwishoni mwa mwezi March,” Jaydee alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
“Na album yenyewe nategemea kuitoa mwezi ujao kwasababu siwezi tena kusubiri zaidi. Ilikuwa itoke mwaka jana mwishoni lakini kutokana na mipangilio kuwa haijakamilika, tukaisogeza mbele ili tufanye kitu kizuri zaidi kwa watu. Kwahiyo wajiandae kwa concert kubwa,” aliongeza.
Jide aliongeza kuwa kabla ya album haijatoka, ataachia nyimbo mbili alizowashirikisha wasanii kutoka nchi za Afrika.
No comments