Usikose Hizi Hapa

SERIKALI KWA USHIRIKIANO WA TAASISI ZA AFYA YAANZA MPANGO WA KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU YA MAGONJWA WA SARATANI KWA WANANCHI

Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Afya Duniani ,imeanza mpango maalum wa kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya awali kwa waathirika wa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti nchini.

Akipokea msaada wa vifaa vya Matibabu vyenye thamani ya Shilingi milioni 98 kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi  kutoka taasisi za USAID,PINCK REBON & RED REBON na JHPIEGO jijini Dar es Salaam,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dokta Ummy Mwalimu amesema katika kulitambua hilo serikali imekuwa na kipaumbele katika suala la Afya hasa katika magonjwa ya Saratani.

Dokta Ummy amesema Serikali imekuwa na jitihada za kutoa matibabu maalum ya wazi katika vituo vyote vya Afya ili kuweza kuwafikia wananchi wengi hasa wanawake katika matibabu ya saratani ya mlango wa uzazi na saratani ya matiti ambayo ndiyo magonjwa  yanaongoza kuuwa wanawake wengi nchini na hadi kufikia mwezi Disemba mwaka huu Serikali itakuwa imewapima wanawake milioni 3.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dr.Ummy Mwalimu akipokea msaada wa vifaa vya matibabu vya magonjwa ya saratani kutoka taasisi za USAID,PINCK REBON & RED REBON na JHPIEGO.

Ameongeza kuwa kuna asilimia 50 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa uzazi pamoja na saratani ya matiti ambapo takwimu zinaonyesha katika wagonjwa 100 wanaofika hospitali ya Ocean Road iliyopo jiji Dar es Salaam,wagonjwa takribani 80 wanakutwa na ugonjwa ukiwa tayaria ameshamuathiri kwa kiasi kikubwa hivyo inawabidi kupata huduma za kuwapunguzia maumivu tu.

''na tusiogope kusema ukweli,kwa sababu lazima watu wajtokeze kufanya uchunguzi wa saratani ili waweze kupata matokeo mazuri''amesema Dr Ummy.

Amefafanua taarifa alizozitoa mwezi uliopita ambapo Dr Ummy ,amesema kuwa Serikali imeendeleza jitihada za kuongeza vituo vya Afya vya uchunguzi na matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi ambapo vilikuwa 343 na sasa vimeongezwa vituo 100 na kufikia 443 katika kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia 2017.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya JHPIEGO, Jeremie Zoungrama amesema lengo la kuisaidia Serikali kutoa vifaa vya matibabu ya magonjwa ya Saratani ni kuhakikisha magonjwa hayo yanapungua kwa kiasi kikubwa hasa katika bara la Afrika.

Hata hivyo Dr Ummy amesisitiza kuwa kufikia mwakani (2018) Serikali inategemea kuaza kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 mpaka 13.


No comments