Video;Magwiji wa soka Man Utd na Barca kukuta dimbani
Wachezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United watavaana na wahenga wenzao wa Barcelona mchezo utakaofanyika jumamosi ya tarehe 2 Septemba mwaka huu kunako dimba la Old Trafford.
Kwenye mchezo huo wakongwe wa Manchester United wataongozwa na Andrew Cole ambapo wachezaji kama Edwin van der Sar, Paul Scholes, Denis Irwin, Dwight Yorke, Phil Neville, Ronny Johnsen, Louis Saha, Mikaël Silvestre, Jesper Blomqvist, Quinton Fortune na Dion Dublin wameshathibitisha uwepo wao.
Kwa upande wa wakongwe wa Barcelona hao wataongozwa na José Mari Bakero kama kocha wao huku wachezaji mwiba kama Gaizka Mendiaeta, Éric Abidal, Migel Angel Nadal, Gheorghe Popescu, Ion Andoni Goikoetxea na Julio Salinas wakithibitisha kushiriki.
Mchezo wa kwanza uliofanyika june 30 mwaka huu, Wahenga wa Manchester United waliwatandika goli 3-1 wakongwe wa Barcelona.
Mechi hiyo yenye lengo la kuchangia mfuko wa Manchester United wa kusaidia watoto wenye vipaji kufikia malengo yao, Tiketi za mchezo huo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha Euro 50 kwa watu wazima na watoto Euro 5.
Tazama mechi ya kwanza jinsi Wahenga wa Barcelona walivyotandikwa na Manchester United.
No comments