Usikose Hizi Hapa

USAJILI: Tetesi za usajili barani Ulaya

Arsenal wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili mchezajiwa Paris Saint-Germain, Lucas Moura. (UOL)
Real Madrid wamemhakikishia, Gareth Bale mwenye umri wa miaka 28, kuwa bado ana nafasi katika klabu hiyo katika hatua ambayo pengine itawahuzunisha Manchester United. (Observer)
Chelsea wana matumaini ya kuwazidi kete Liverpool katika kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Evening Standard)
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa “hawana nafasi yoyote” na kumsajili beki kutoka Brazil, Alex Sandro, 26. (ESPN)
Chelsea wanaonekana kuwa tayari kupambana vikali na Manchester United katika kumsajili, Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Sunday Express)
Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 120 kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho. (Star on Sunday)
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp tayari anapanga kumsajili, Manuel Lanzini kutoka West Ham kuziba pengo la Philippe Coutinho. (Mundo Deportivo)
Antonio Conte amesema hana nguvu zozote za kuzuia Chelsea kumuuza, Eden Hazard. (Sunday Mirror)
Barcelona wanamtaka kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast, Jean-Michael Seri, 26, anayechezea Nice, ambaye pia anasakwa na Arsenal. (Mundo Deportivo)
Matumaini ya Liverpool kumsajili kiungo wa Rennes, Benjamin Andre, 27, yamefifia. (Sunday Express)
Tokeo la picha la Rennes, Benjamin Andre
Newcastle wanamtaka kipa wa West Ham Adrian, 30, ili kuimarisha safu yao ya makipa. (Sky Sports)Mnunuzi ambaye bado hajafahamika kutoka China ameonesha nia ya kutaka kununua baadhi ya hisa za Manchester United. (Sunday Times)
Barcelona wapo tayari kuwatoa wachezaji wake, Andre Gomes na Rafinha kama sehemu ya mkataba wa kumsajili, Paulo Dybala kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport)
Everton wanamfuatilia mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck mwenye umri wa miaka 26, iwapo watashindwa kumshawishi, Olivier Giroud, 30, kuondoka Emirates. (Sunday People)
Meneja wa Everton, Ronald Koeman ana matumaini ya kumsajili beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen mwenye umri wa miaka 31, kutoka Barcelona. (Sun on Sunday)
Tokeo la picha la Arsenal, Thomas Vermaelen
Swansea lazima walipe pauni milioni 13 ikiwa wanataka kumsajili tena Wilfried Bony kutoka Manchester City. (Sunday Mirror)
Meneja wa Borussia Dortmund Peter Bosz amesema hana wasiwasi kuhusu kumpoteza mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20, anayenyatiwa na Barcelona. (Metro)
Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumsajili kiungo wa Tottenham, Dele Alli mwenye umri wa miaka 21, baada ya kumuuza, Neymnar kwa pauni milioni 200. (Sunday Express)
Tokeo la picha la Tottenham, Dele Alli
Bayern Munich wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa Tottenham, Eric Dier mwenye umri wa miaka 21. (Sun on Sunday)
Arsenal, Liverpool, Manchester City na Barcelona wapo katika vita nzito ya kumuwania kiungo wa AS Monaco, Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 21. (Sunday Mirror)
Manchester United na Chelsea wanafikiria kumsajili kiungo wa Barcelona, Sergi Roberto. (Don Balon)

No comments