Video: Napenda kitu anachofanya Alikiba – Ebitoke
Mchekeshaji kutoka Timamu Media Africa, Ebitoke amedai kuwa anapenda kile anachofanya msanii wa Bongo Flava, Alikiba na wimbo wowote atakaoutoa yeye ataupokea kwa mikono miwili.
Ebitoke ameeleza kuwa yeye ni shabiki wa kutupwa wa msanii huyo na ndio sababu ya kumkubali na atakapopata fursa ya kumshauri atamshauri vitu vizuri.
“Kwa upande wangu mimi nampenda Alikiba, mimi ni shabaiki wake, ngoma yake yoyote akitoa kwa upande wangu naizungumzia fresh, naipokea vizuri kwa sababu mimi napenda kitu chake anachofanaya,” Ebitoke ameiambia Bongo5.
Alipoulizwa akikutana na Alikiba atamshauri kitu gani, Ebitoke alijibu, “Nitamshauri kwanza awasikilize mashabiki zake, atusikilize sisi kitu tunachopenda na vile vile aendelee katika kazi zake na misimamo yake asisikilize maneno ya watu wabaya yatakayomfanya aumie, kwa hiyo ajikite katika kazi zake na kuongeza ubunifu,” amesema.
Ebitoke ambaye amekuwa akibamba zaidi katika uchekeshaji pindi anapoigiza na Mama Ashura amekuwa akimkingia kifua Alikiba katika muziki wake, huku Mama Ashura akiukosoa vikali mtindo wa Alikiba katika muziki na kuweka wazi zaidi mahaba yake ya kimuziki kwa Diamond Platnumz.
>>>>>>HABARI KUTOKA BONGO 5<<<<<<<
No comments