Maamuzi ya Mahakama kuu kuhusu dhamana ya Manji
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam Leo imeyatupilia mbali maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na DPP.
Maombi hayo yametupiliwa mbali na Jaji Isaya Arufani.
Kabla ya kutupiliwa mbali, maombi hayo, Manji alisimama na kuieleza mahakama kukataa kuwakilishwa na Wakili Peter Kibatala kwa sababu za kisiasa.
Amedai, alipopeleka maombi ya dhamana alimpa maelekezo wakili Joseph Tedayo lakini alishangaa kesi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kisikilizwa maombi yake ya dhamana wakili Kibatala ndiyo alifika kumuwakilisha.
Kutokana na hayo, Manji ameiomba Mahakama mawakili, Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Seni Malimi ndio wawe wanamuwakilisha katika maombi hayo.
Hivyo DPP akiwakilishwa na mawikili Paul Kadushi na Simon Wankyo walidai kuwa, wamesilisha kiapo kinzani kupinga maombi hayo ya dhamana wakiwa na hoja tatu.
Hoja hizo ni kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo ya dhamana na kwamba yanapaswa kusikilizwa na mahakama ya kifisadi kwa kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi.
Ameongeza kiqa vifungu vya kisheria vilivyotumika kuleta maombi hayo siyo sahihi na pia hati ya kiapo iliyoambatanishwa kuunga mkono maombi hayo ina dosari kisheria ambazo haziwezi kurekebishika.
Kadushi aliiomba mahakama kusikiloza kwanza mapingamizi ya DPP kabla ya kuanza kusikiliza maombi ya dhamana.
Hata hivyo Wakili Mgongolwa akiwakilisha jopo la mawakili wa Manji walikubaliana na mapingamizi ya DPP kuwa ni kweli yana msingi na maombi ya dhamana yanadosari.
Kufuatia kukiri huko, Kadushi aliiomba mahakama kutupilIa mbali maombi hayo ya dhamana.
Akitoa uamuzi, Jaji Arufani amekubaliana na mleta Maombi (Manji) kuwa hawakilishwi na Kibatala. Pia amesema mahakama kuu haina mamlaka ya kusikiliza maombi hayo hivyo ameyatupilia mbali.
Katika maombi hayo ya dhamana, Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurgenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Kwa mujibu wa hati ya maombi hayo, Manji anadai kuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo na kwamba ameambatanisha vyeti vya daktari katika maombi yake.
Katika kesi ya msingi, Manji na wenzake wanatuhumiwa kukutwa na mihuri ya mbalimbali ya JWTZ isilivyo halali vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 236.5.
Mbali na Manji, washtakiwa wengine ni, Ofisa Rasilimaliwatu Deogratias Kisinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Mtunza Stoo msaidizi, Thobias Fwele (43)
No comments