Jinsi Ya Kujifunza Utabibu Wa Asili!
Kwa muda mrefu sasa, nimekuwa nikipokea simu, ujumbe mfupi wa maneno (sms) pamoja na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, kutoka hapa nchini na nchi jirani, wakiomba kujifunza UTABIBU WA ASILI.
Katika miaka ya hivi karibuni, watu wengi wamekuwa na muamko mkubwa sana kuhusu tiba za asili.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tiba za asili zimethibitika kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutibu na kuponyesha magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya yanayo mkabili mwanadamu.
Kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya watu wenye uhitaji mkubwa na endelevu wa tiba za asili, watu wengi kutoka sehemu mbalimbali wamekuwa wakitafuta namna ya kujifunza kuhusu utabibu wa asili, ili wapate maarifa yatakayo wasaidia kuanzisha huduma ya tiba asilia, ambayo mbali na kuwasaidia katika kuendesha maisha yao ya kila siku, lakini pia itawapa uwezo wa kuwasaidia watu mbalimbali wenye kusumbuliwa na magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.
MAHALI UNAPOWEZA KUJIFUNZA UTABIBU WA ASILI
Kwa mujibu wa SHERIA YA TIBA MBADALA YA TANZANIA, mtu anaweza kuwa tabibu wa asili eidha kwa kujifunza au kwa kurithishwa.
i. Anaweza kurithishwa na baba, babu, bibi nakadhalika.
ii. Anaweza kujifunza kwenye chuo rasmi. Tanzania mafunzo rasmi ya tiba mbadala hutolewa pale Muhimbili kwenye kitengo au Taasisi ya Tiba za Asili iliyopo pale Muhimbili.
Mafunzo yanatolewa kuanzia ngazi ya cheti na kuendelea, na hutolewa kwa wanafunzi walio timiza vigezo kama vile kufaulu vizuri somo la Baiolojia kwenye mtihani wa kidato cha nne au cha sita.
iii. Tatu; Anaweza kujifunza kwa MGANGA AU TABIBU WA ASILI.
Baraza la Tiba Asilia na Tiba Mbadala litamtambua na kumsajili, tabibu ambae amepata mafunzo yake katika moja wapo kati ya sehemu nilizo zitaja hapo juu.
Toka enzi za mabibi na mababu, matabibu wengi wamekuwa wakijifunza kuhusu UTABIBU kupitia kwa matabibu wengine.
Hapa kijana anae taka kuwa tabibu, huenda nyumbani kwa tabibu na kuomba kufundishwa kuhusu utabibu.
Tabibu atamchukua kijana huyo na kuanza kumfunza utabibu kwa nadharia na vitendo mpaka pale atakapo jiridhisha kuwa kijana huyo ameiva kwenye utabibu ndipo atakapo mtawaza utabibu .
Mara nyingi wazazi wa kijana ndio walio mpeleka kijana wao kujifunza utabibu kwa faida yake na ya familia na ukoo kwa ujumla.
Ilikuwa ni jambo la heshima na fahari kuu kutoka katika familia yenye Tabibu wa asili, ambae aliwasaidia watu wenye kusumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Maarifa haya yalisambazwa kizazi hata kizazi.
DOKTA.MUNGWA KABILI NA MAFUNZO YA UTABIBU!
Watu wengi wenye kuvutiwa na kazi ya utabibu wamekuwa wakinipigia simu kuniuliza kama nami pia hutoa mafunzo ya utabibu. Jibu langu ni NDIO.
Toka mwaka 1987, nimekuwa nikitoa mafunzo haya kwa watu mbalimbali wenye kuvutiwa na kazi ya utabibu.
Mamia ya matabibu wa asili, wamepitia kwenye mikono yangu. Wengine wamejifunza utabibu kilingeni kwangu, wengine wamejifunza kwa njia ya masafa marefu.
Kila mwaka huwa ninatoa mafunzo ya utabibu kwa idadi kadhaa ya vijana wa kike kwa kiume, ambao wanavutiwa na kazi ya utabibu .
Mafunzo ninayo yatoa ni yale ya JINSI YA KUTIBU NA KUPONYESHA MAGONJWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI.
Vijana hawa hujifunza kuhusu maelfu ya aina mbalimbali za dawa za asili, kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na Afrika kwa ujumla, bila kusahau dawa za asili kutoka uarabuni na India.
Sifa za kupata nafasi ya kufundishwa nami kuhusu utabibu wa asili, ni kwanza uwe na wito wa kufanya kazi ya utabibu, pili uwe na akili timamu, tatu uwe unajua kusoma kuandika na nne uwe raia mwema, tano uwe na nidhamu.
Kama una wito na kazi ya utabibu na unataka kujifunza kuhusu utabibu, basi wasiliana nami kwa simu namba 0744 000 473.
Vile vile wapo wazazi na walezi ambao wamekuwa wakinipigia simu, wanasema watoto wao wapo tu mtaani, hawana kazi za kufanya, je wanaweza kuwaleta kwangu wajifunze utabibu?
Jibu langu ni, kazi ya utabibu ni kazi inayo hitaji wito ndani yake. Sio kazi ya kufanya kwa sababu hauna kitu kingine cha kufanya. Ni kazi ambayo inatakiwa kufanywa na mtu anae ipenda kutoka moyoni. Usikimbilie kuifanya kazi hii kwa sababu unajua ina maslahi makubwa ndani yake. Kwanza uwe na wito ndani yako.
IMESIMULIWA NA DOKTA MUNGWA KABILI 0744 000 473.
No comments