Usikose Hizi Hapa

MEEK MILL AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 2-4 JELA

Meek Mill amehukumiwa kwenda jela? Rapper huyo amekutana na rungu la kifungo cha miaka 2-4 jela.
Jaji wa mahakama ya mjini Philadelphia amemhukumu mwandishi huyo kifungo hicho kutokana na kukiuka masharti ya majaribio yake ya kesi ya madawa ya kulevya na silaha ya 2009.
Hukumu hiyo imetolewa Jumatatu hii ambapo rapper huyo alionekana mahakamani hapo. Hukumu hiyo imekuja baada ya kukamatwa kwa kosa la kupigana kwenye uwanja wa ndege wa St. Louis na kuendesha gari kwa fujo mjini New York City.
Baadhi ya watu akiwemo Jay Z wamelaani hukumu hiyo wakidai kuwa imemuonea Meek.

No comments