Usikose Hizi Hapa

REFA ELLY SASII KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA SEVILLA ALHAMISI UWANJA WA TAIFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza Waamuzi watakaochezesha mchezo wa kirafiki wa kimataifa Simba dhidi ya Sevilla ya Hispania itakayochezwa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Alhamisi wiki hii.


Muamuzi wa katikati atakua Elly Sasii, Muamuzi msaidizi namba moja Mohammed Mkono kutoka Tanga, muamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila wa Dar es Salaam na Muamuzi wa akiba atakuwa Jonesia Rukyaa kutoka Kagera.


Sevilla wanatarajia kuwasili Kesho Jumanne ikiwa na msafara wa watu 62.

Mbali na mchezo huo utakaochezwa Alhamis saa 1 usiku Sevilla watafanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa pamoja na kuendesha semina ya Uongozi kwa Vilabu.


Kiingilio katika mchezo huo PlatInum shilingi 100,000,VIP B 15,000 na Mzunguko 5,000.

Simba imepewa nafasi ya kucheza na Sevilla kwa kigezo cha Klabu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa Cup kwa timu zinazodhaminiwa na SportPesa.


Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred alisema kigezo kikubwa kilichotumika kuchagua timu ya kucheza mchezo huo ni timu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa ambapo Simba ilifikia hatua ya nusu fainali.


Amesema ratiba ya Ligi Kuu imebana kimetumika kigezo cha mashindano ya SportPesa kumpata muwakilshi wa kucheza na Sevilla.

No comments