Usikose Hizi Hapa

RUBY AELEZA ANACHOKIPENDA KUTOKA KWA JUX

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amefunguka kuhusu kuvutiwa na Jux kwa upande wa uimbaji wake.
Muimbaji huyo ameiambia Clouds Fm kuwa amekuwa akivutiwa zaidi na wimbo wa Jux unaokwenda kwa jina la Utaniua.
“Kwa sababu nyimbo za Jux karibia zote zinawashika kwanza wanawake, halafu pia uimbaji wake ni RnB ambayo anaweza kuimba mwanaume au mwanamke, kwa hiyo nafikiri ule uliniingia zaidi,” amesema Ruby.
Ruby kwa sasa anafanya vizuri kwa sasa na ngoma ‘One and Only’ aliyoshirikishwa na Nedy Music.

No comments