MAREKANI KUONGEZA WANAJESHI MASHARIKI YA KATI
Wizara ya ulinzi ya Marekani inaangazia ombi la jeshi la nchi hiyo la kupeleka wanajeshi 5,000 zaidi Mashariki ya Kati, wakati wasiwasi ukiongezeka kati yake na Iran.
Kulingana na maafisa wawili waliozungumza na shirika la habari la Reuters kwa masharti ya kutotajwa majina, ombi hilo limewasilishwa na makao makuu ya jeshi la Marekani, lakini bado haiko wazi iwapo wizara hiyo italiidhinisha.
Mmoja wa maafisa hao amesema wanajeshi hao wanapelekwa kwa ajili ya kujihami.
Hili linatajwa kama ombi la karibuni zaidi la kuongezwa kwa wanajeshi katika kile ambacho Marekani inakitaja kama kitisho dhahiri kutoka kwa Iran dhidi Marekani na maslahi yake katika ukanda wa Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, wizara hiyo ilipoulizwa ilikataa kuzungumzia mipango yake ya usoni.
No comments