Usikose Hizi Hapa

MAKAMBO ; NASEPA YANGA MAZIMA ,NITAWAKUMBUKA DAIMA

Mshambuliaji tegemeo wa kikosi cha Yanga, Heritier Makambo amesema kuwa anaumia kuondoka Yanga kwa kuwa kuna vitu vingi atavikumbuka ila hamna namna ni lazima aondoke kwa kuwa kila kitu kimekamilika nchini Guinea.

Makambo mwenye mabao 17 ndani ya ligi anakwenda kujiunga na Horoya AC ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutwaa ubingwa msimu huu amesaini mkataba wa miaka mitatu.


"Mambo yangu yote na Horoya yameshaisha, hivyo ni lazima niondoke Yanga hamna namna nyingine, nitawakumbuka mashabiki wa Yanga namna wanavyoipenda Yanga na namna walivyokuwa nasi bega kwa bega, ninaondoka ila nitawakumbuka" amesema Makambo.

No comments