One the Incredible--Nilijua mashabiki watachoma albamu zangu zote
Msanii wa hip hop Bongo, One the Incredible amesema wakati anaachia ngoma yake ya Danga ambayo amewashirikisha Diamond Boys kutoka Zimbabwe hakutarajia angepata mapokezi makubwa kama ilivyo sasa.
Rapper huyo amekiambia kipindi cha Ladha 3600 cha E FM, mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa na kufika sehemu ambayo hata hakutarajia.
“Kwa upande wangu binafsi nilitengemea katika ngoma ambazo watu wangeongea sana ilikuwa ni Danga, nilijua kabisa kuna watu hapa ndio watachoma albamu zote sio moja lakini cha kushangaza nimepata support,” amesema One na kuongeza.
“Watu wanashare, wanatuma meseji za big up wanaonyesha wameipenda ngoma, na hata kwa rate ya downloads ambazo nimepata kwenye hii ngoma inaonyesha imefika mbali, umefikia hata watu ambao sikutengemea wanaweza kusikiliza muziki wangu, kwa hiyo Danga imefika mahali pake,” amesisitiza.
No comments