Chemical azungumzia kivazi chake kilichoibua gumzo
Chemical amefunguka baada ya watu kuhoji kivazi alichovaa katika video mpya ya Msamii ‘So Fine’.
Rapper huyo amesema kuwa yeye ndiye bosi wa muziki wake na pia watu waelewe kuwa sanaa ni zaidi ya mavazi na shabiki anapaswa kujielekeza zaidi katika kazi ya msanii, lakini wale waliokosoa muonekano wake sio kitu kilichomkwaza.
“Hapana siwezi kuwa disappointment kwa sababu mimi nilivyojitambulisha kwa watu walinikubali jinsi nilivyo, kwa hiyo ningeamua kujitambulisha kwa namna ile watu walivyoniona na Msami pia watu wangekubali kwa sababu walikuwa hawajui the real me, kwa hiyo vyote vyote ningeamua kujionyesha kwa mashabiki wangenikubali,” ameiambia Daladala Bets ya Magic Fm na kuongeza.
“Kitu kingine nilitaka kuonyesha kuwa mavazi sio kitu kikubwa katika sanaa, naweza kubalika vyovyote ninavyotaka kuwa, mwisho wa siku unachatakiwa kupokea kutoka kwangu ni muziki,” amesisitiza.
No comments