TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMATATU MEI 20
Streka wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebainisha kuwa anaweza kuihama klabu yake katika kipindi hiki cha usajili. Kauli hiyo inatarajiwa kuziamsha klabu kongwe na tajiri kama Real Madrid, Barcelona na Manchester City kumgombea. (Express)
Kiungo raia wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28, anataka kurudi mezani na klabu yake ya Manchester City kwa malengo ya kusalia klabuni hapo zaidi ya mwezi Juni 2020 ambapo mkataba wake wa sasa unaishia. (Mail)
Kocha Pep Guardiola atapewa fursa ya kusalia klabuni Manchester City walau kwa miaka mitano ijayo huku kipato chake kikifikia pauni milioni 100, baada ya mshahara wake kwa mwaka kuchupa toka pauni milioni 15 mpaka milioni 20. (Sun)
Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, ambaye anakipiga kwenye ligi kuu ya Uchina, klabu ya Dalian Yifang, anataka kuhamia katika ligi ya Primia na Arsenal wanatarajiwa kumnyemelea, klabu hiyo ilikaribia kumsajili katika dirisha dogo la usajili la Januari. (Sun)
Arsenal pia wanamnyemelea beki wa kati na kinda wa timu ya Saint-Etienne na timu ya taifa ya chini ya miaka 19 ya Ufaransa, William Saliba, 18. (Goal.com)
Mshambuliaji aliyepoteza kiwango wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, anatarajiwa kukatiza mapumziko yake ya mwisho wa msimu na kurudi klabuni ili kujifua na kujihakikishia nafasi katika kikosi cha United. (Sun)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwonesha dalili za wazi winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, kuwa muda wake katika klabu hiyo umefikia tamati, baada ya kusema kuwa asingemuingiza mchezoni kutoka benchi walipofungwa Jumapili na Real Betis hata kama kungekuwa na fursa ya kuingiza wachezaji wanne. (Eurosport)
Bale hata hivyo amewaambia wachezaji wenzake kuwa anapanga kusalia klabuni hapo mpaka kwisha kwa mkataba wake na takuwa mwenye furaha kucheza gofu endapo hatapangwa kucheza. (Radioestadio, via Mail)
Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 28, anapiga hessabu za kuikacha klabu yake na kujiunga na miamba ya Ligi ya Ufaransa PSG. (Talksport)
Manchester United watarasimisha nia yao ya kumsajili kiungo wa Lyon, Tanguy Ndombele, 22, pale tu mustakabali wa kiungo wao Paul Pogba, 26, utakapokuwa wazi. (Manchester Evening News)
Kocha wa Lille, Christophe Galtier amethibitisha kuwa winga raia wa Ivory Coast winger Nicolas Pepe, 23, ataihama klabu hiyo hivi karibuni. Mcezaji huyo anahusishwa na uhamisho na klabu kongwe za Manchester United, Arsenal na Bayern Munich. (Manchester Evening News)
No comments