TAFITI: ENDAPO BANGI ITAHALALISHWA ITAOKOA MAISHA YA WATU 50,000 KWA MWAKA
Wahenga walisema kila chenye kasoro hakikosi faida! Kwa nchi za Afrika ni kosa kubwa kukutwa unatumia madawa ya kulevya aina ya bangi ingawaje kuna baadhi ya nchi kama Kenya, Nigeria na Afrika Kusini zinapambana kuruhusu majani hayo kutumiwa kama zao la biashara.
Sasa watafiti kutoka chuo Kikuu cha Indiana nchini Marekani wamekuja na majibu ya tafiti kuwa utumiaji wa bangi hauna mathara makubwa ukilinganisha na faida zake mwilini na kudai kuwa endapo serikali nchini Marekani itaruhusu utumiaji wa mmea huo itapunguza vifo 50,000 kwa mwaka.
Watafiti hao wamesema kuwa wengi wanaamini watumiaji wa bangi ni wezi, wahuni na watu wenye tabia mbaya lakini ni tiba kwa watu waliopatwa na msongo wa mawazo, Wanaonyemelewa na magonjwa ya Kansa, na kuokoa vifo vya mapema vinavyotokana na magojwa ya unene kupitiliza na kudai kuwa endapo bangi itaruhusiwa nchini humo (Marekani) kwenye majimbo yote itapunguza vifo vya watu elfu 50.
Utafiti huo ulitumia watu elfu 60 wanaosumbuliwa na msongo wa mawazo, presha kutoka Marekani ulikuja na matokeo chanya. Ambapo watu elfu 30 walikiri hupata nafuu kila wanapotumia mmea huo. Huku watu elfu 15 wakisema huwa wanatumia madawa hayo kwa ajili ya kushindwa kuyaacha ila hayana faida wala hasara kwenye kwenye miili yao.
Watu elfu 15 wamesema hawajui chochote kuhusu mjani huo kuwa ni dawa, ila endapo utathibitishwa na madaktari watakuwa tayari kutumia.
“Utafiti umeonesha kuwa bangi inapunguza vifo vya mapema kwa kupunguza presha, Ukali wa magonjwa ya kansa na kupoteza kabisa msongo wa mawazo ambapo kwa sasa vifo vinavyotokana na magonjwa hayo vinaongezeka kila mwaka na tayari mpaka sasa nusu mwaka zaidi ya watu elfu 30 wamepoteza maisha kutokana na magonjwa hayo na mengine yanayoshabihiana, Tunaamini serikali itaruhusu majimbo yote (nchini Marekani) kuanza kutumia bange kuepuka vifo vinavyozuilika,“imeeleza tafiti hiyo iliyochapwa na jarida la Reddirt REPORT.
Utafiti huo awali ulipata pingamizi kutoka kwa mtaalamu wa masuala elimu ya viumbe, Prof. Thomas Clark kwa kudai kuwa utafiti ungeangalia zaidi jinsi ya bangi inavyoweza kuongeza umri wa kuishi ila sio kwenye vifo kwani kila mwaka Marekani inapoteza zaidi ya elfu 50 kwa vifo vinavyotokana na madawa ya kulevya.
Kwa mujibu wa takwimu za uhalifu zilizotolewa mwaka jana 2016 nchini Marekani na FBI zinaonesha nchi hiyo inakamata watumiaji bangi laki 6 na hupoteza kiasi cha dola bilioni 3 kuwahudumia hivyo endapo utafiti huo utakuwa na manufaa huenda Marekani ikaruhusu mjani huo kuwa dawa rasmi.
No comments