Usikose Hizi Hapa

BARCA WAPOKEA KIPIGO KUTOKA KWA VALENCIA USIKU FAINALI YA KOMBE LA MFALME

Kevin Gameiro na Rodrigo walfunga magoli mawili huku Valencia ikiwalaza mabingwa wa La Liga Barcelona kushinda taji la Copa del Rey.
Kikosi cha Ernesto Valverde kilisema katika maandalizi yao kwamba ushindi utasaidia kuponya majeraha waliopata walipolazwa na Liverpool katika kombe la mabingwa, lakini walishindwa kung'ara mbele ya Sevilla.
Mshambuliaji wa Ufaransa Gameiro alifunga goli zuri na kuipatia Valencia bao la kwanza kabla ya Rodrigo kufunga bao la pili kupitia kichwa.
Bao la dakika ya 73 la Lionel Messi liliwapatia matumaini Bareclona lakini wakashindwa kusawazisha.
Kevin Gameiro
Kevin Gameiro alifunga goli lake la nne katika mechi nne akiichezea Valencia
Baada ya mechi hiyo rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu alimuunga mkono kocha Valverde kuendelea kuiongoza klabu hiyo.
''Nimekuwa nikisisitiza kuwa Ernesto ana kandarasi katika msimu ujao , yeye ndio kocha'', alisema.
''Sidhani kwamba kichapo hiki kilisababishwa na makosa ya mkufunzi''.
Valverde alisema: "Wakati kocha anaposhindwa anataka kuendelea tena ili kukabiliana na changomoto nyengine inayomkabili mbele yake. Najua ni vigumu kushindwa katika klabu hii''.
Kulikuwa na ishara ya matumaini katika dakika ya nane wakati ambapo beki wa Barcelona Clement Lenglet alinusurika adhabu ya makosa yake.
Pasi yake mabaya ilichukuliwa na Rodrigo , lakini kwa bahati nzuri beki Gerard Pique alikuwa karibu ili kuondoa hatari hiyo iliokuwa karibu na laini ya goli.\
Hatahivyo kulikuwa hakuna cha kulizuia goli la Gameiro kufuatia kupa nikupe nzuri kutoka kwa Jose Gaya.
Beki huyo wa kushoto alimpigia pasi nzuri mshabuliaji huyo wa Ufaransa ndani ya boksi kabla ya kupiga mkwaju ambao uliingia katika paa la kipa Jasper Cillessen.
Dakika 12 baadaye , Rodrigo, ambaye alisababisha matatizo katika safu ya ulinzi ya Barca alifunga krosi ya Carlos Soler.
Messi, ambaye mara nyengine hujipoteza katika mechi alimjaribu kwa mashambulizi kipa wa Valencia Jaume Domenech kwa mara ya kwanza kabla ya kipindi cha pili na akafanikiwa baada cha kipindi ya pili.
Mkwaju wa mshambuliaji huyo wa Argentina uligonga mwamba na kutoka nje kabla ya shambulizi lake jingine kuokolewa na mkono mmoja na kipa huyo.
Messi hatahivyo alicheka na wavu baada ya kufunga goli lake la 28 dhidi ya Valencia katika mashindano yote.
Kichwa che Pique kutoka kona kiligonga mwamba na kurudi uwanjani huku mchezaji huyo nambari 10 mgongoni akifunga kwa urahisi karibu na goli.
Hatahivyo licha ya Messi na timu yake kuvamia lango la Valencia kunako dakika 15 za mwisho , ni mchezaji wa Valencia Goncalo Guedes ambaye karibu afunge magoli mawili.
Ushindi huo unamaanisha kocha Marcelino Garcia Toral alisitisha msururu wa kibinafsi wa mechi 20 bila kushindwa katika michuano yote dhidi ya Barcelona.

No comments