Harmonize apata ‘kwikwi’ gharama za mjengo wake
Msanii wa Muziki Bongo, Harmonize ameshindwa kuweka wazi gharama alizotumia hadi sasa katika nyumba yake anayojenga.
Muimbaji huyo kutoka label ya WCB, amesema ndio kwanza anaanza na Mungu akijalia mwakani mwishoni inaweza ikawa imeisha na nyumba hiyo ni ghorofa.
“Kwa hiyo flow ya kwanza tayari bado ya pili, kidogo kidogo tunajikongoja tukipata 200 tunaweka. Sio kitu kizuri kusema (gharama) nadhani lakini imetumia hela nyingi,” ameimbia XXL ya Clouds Fm na kuongeza.
“Siwezi nikakadiria lakini imekula hela nyingi, show zenyewe hizi kwa mwaka sita/saba na usawa wenyewe ulivyo mgumu lakini nashukuru sio show pekee zinazonipatia hela kuna mishe nyingine, kwa hiyo siwezi kujua ni kiasi gani imekula lakini imekula hela nyingi,” amesema Harmonize.
Harmonize kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sina’ ambayo katika video yake amemshirikisha msanii mwenye heshima yake katika Bongo Flava, Mr Nice.
No comments