Rais alichokitegemea kwangu siyo kile anachokiona – Waziri Mwijage
Baada ya Rais Magufuli kumuagiza Waziri wa viwanda,Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage kuwachukulia hatua watu waliouziwa viwanda na kisha kuvitelekeza. Waziri Mwijage amesema kuwa Rais alichokitegemea kwake siyo kile anachokiona kwa sababu viwanda haviendi kwa kasi anayoiona.
Waziri Mwijage ameyazungumza hayo leo katika kipindi cha Clouds 360kinachorushwa na Clouds TV ambapo amesema kuwa sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, Vingine maliasili.
“Kujenga viwanda siyo mchezo yapo maelekezo ya Mh Rais viwanda vilivyo binafsishwa na havitumiki virudishwe. Rais alichokitegemea kwangu siyo kile anachokiona kwa sababu Viwanda haviendi kwa kasi anayoiona na hii ni kutokana na sababu kadhaa hii sekta ya viwanda ni multi-sector maana kuna viwanda vipo chini ya Wizara ya Mifugo, Vingine maliasili,” amesema Waziri Mwijage.
Aidha Waziri Mwijage alisema kuwa “Siwezi kumsemea Mhe. Rais najua ana imani na mimi sana, ndiyo maana nilimuomba asinikumbushe tena siku nyingine.Kiwanda cha General Tyre, kina historia kubwa zaidi kilikuwa cha jumuiya ya Afrika Mashariki lakini sasa ni mali yetu.”
No comments