Tuna mengi ya kujifunza uchaguzi wa Kenya – Halima Mdee
Kufuatia uchaguzi unaoendelea Kenya, Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee amepongeza uchaguzi unaoendelea nchini Kenya huku akisema kuwa wananchi wana mengi ya kujifunza katika uchaguzi huo.
Halima Mdee amebainisha hayo kupitia ukurasa wake twitter huku akisema Kenya ni majirani zetu lakini wametuacha mbali.
Kama tuna akili timamu!! Tuna mengi sana ya kujifunza katika uchaguzi wa Kenya . Ni majirani zetu, lakini wametuacha mbali sana.
Hata hivyo suala la wafungwa kupiga kura nchini humo ni mara ya kwanza tokea kubadilishwa kwa Katiba yao jambo ambalo limewatamanisha watu wengi kutoka Tanzania nao kutaka wafungwa waliopo kwenye vifungo wapige kura.
Mpaka sasa Rais Uhuru Kenyatta kutoka muungano Jubilee anaongoza kwa kura 6,574,087 sawa na (55.21%) akifuatwa na Raila Odinga kutoka muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) akiwa na kura 5,236,724 (43.98%).
No comments