Usikose Hizi Hapa

VIDEO;BAADA YA KUICHAPA BAYERN,LIVER YAKIONA CHA MOTO KWA ATRETICO...

Hatimaye majogoo wa jiji la London maarufu,Liverpool fc wamefungwa na klabu ya Atretico De Madrid kwa nikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 dimba la Allianz Arena nchini Ujerumani katika michuano ya kirafiki inayoendelea ijulikanayo kama Final Audi Cup 2017 usiku wa kuamkia jana.

Atretico walianza kupata bao dakika ya 33 kupitia kwa mchezaji Keid Bare wakati goli la Liverpool lilifingwa na mchezaji Roberto Firmino kwa mkwaju wa penati dakika ya 83 baada ya mchezaji Divork Origi kuangushwa katika eneo la penati.

Kapteni Jordan Henderson ndiye aliyeshusha majonzi kwa mashabiki wa Liverpool baada ya kukosa mkwaju wa penati na hatimaye Atretico kuibuka washindi kwa penati 5-4 katika mchezo huo.
TAZAMA MECHI YA ATRETICO MADRID NA LIVEPOOL

Hii ni baada ya Liverpool kutoa kipigo kitakatifu kwa klabu ya Bayern Munich cha mabao 3-0 usiku wa kuamkia juzi, mabao yakifungwa na Sadio Mane,Mohamed Salah na Daniel Sturridge aliyeumia mguu mara tu alipofunga goli la tatu.

TAZAMA MECHI YA BAYERN MUNICH NA LIVERPOOL

No comments