Nataka Tanzania iwe kama Ulaya – Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemaliza ziara yake ya mikoa minne mkoani Singida kwa kuwaahidi watanzania kuwa malengo yake ni kuifanya Tanzania kuwa kama Ulaya.
Akiongea na wananchi wa Itigi mkoani Singida leo mchana Rais Magufuli amesema kwa sasa yupo mbioni kuhimiza ujenzi wa viwanda nchini pamoja na kuziba nyufa zote zilizoachwa na waliomtangulia ingawaje amekiri kuwa ni kazi nguvu.
“Nataka hii Tanzania iwe Ulaya, na tutafika, lakini ili tufike huko ni lazima tutabanana kwelikweli, “,amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema anaumia sana kwa watu walio binafsisha viwanda kwani wamelirudisha taifa nyuma kwa kiasi kikubwa ndiyo maana bado mpaka leo anahangaika kuvifufua viwanda vilivyokufa kutokana na ubinafsishaji.
“Suala la ubinafsishaji mimi silipendi, siwezi nikawalaumu waliofanya haya lakini siwezi nikaacha kusema, Ni lazima niyatapike haya, nikikaa nayo nitapata presha, na wale walioyafanya wakumbuke madhambi yao”,amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya mikoa minne ya Singida, Kigoma, Tabora na Kagera ambako amezindua na kufungua miradi mikubwa 9 ya barabara na Uwanja wa ndege.
No comments