Rich Mavoko adai anafurahia maisha ya WCB, aeleza jinsi anavyoishi na wasanii wenzake
Ikiwa ni miezi 9 toka mkali wa wimbo ‘Kokoro’ Rich Mavoko asaini WCB, amefunguka na kueleza maisha anayoishi ndani ya label hiyo ambayo iko chini ya Diamond Platnumz.
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Rich Mavoko amedai maisha ya WCB ni mazuri na anaishi na wasanii wenzake kwa upendo na kushirikiano ingiwa migongano haikosi.
“Kusema kweli maisha ni mazuri sana, tunaishi kwa upendo, tunashirikiana, ni sehemu ambayo unaweza ukakaa na kufanya muziki nzuri kwa sababu watu ambao wanakuzunguka ni wasanii hata mabosi wetu, Sallam na Tale ni watu ambao wako kwenye huu muziki wa muda mrefu,” alisema Rich Mavoko.
Kwa upande wa muziki wake muimbaji huyo amedai mpaka sasa ameona mafanikio makubwa katika muziki wake hasa hasa kimataifa zaidi kwa kuwa nyimbo zake nyingi zinachezwa kimatifa.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa kolabo zake za kimataifa.
No comments