Yusufu Manji Afikishwa Mahakamani Mchana wa leo
Mfanyabiashara maarufu nchini na mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji amefikishwa mahakamani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka moja la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine..
Manji amefikishwa mahakamani leo ikiwa ni siku ya nane tangu alipojisalimisha na kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alopoitikia wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ili kuhojiwa.
Umati mkubwa wa watu wanaodhaniwa kuwa ni mashahabiki wa Klabu ya Yanga, ndugu jamaa na marafiki wamefurika katika chumba cha mahakama
No comments