Arsene Wenger, hatima yake kujulikana leo
Kocha wa Arsenal, Arsenal Wenger akishangilia Ubingwa kwa kuinua juu kombe la FA, na mmliki wa klabu hiyo mwenye suti nyeusi (kulia) Stan Kroenke akimpongeza
Kocha wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger, amefanya mkutano muhimu na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke siku ya jana ambapo mustakabali wa mfaransa huyo ulitarajiwa kujadiliwa.
Matokeo ya mkutano huo bado hayajawekwa wazi, lakini maamuzi yanabaki baina ya Wenger na Kroenke na yatategemea pia kikao cha bodi kitakachojadili suala hilo leo hii.
Kocha wa Arsenal, Arsenal Wenger akipeana na mikono na mmliki wa klabu hiyo Stan Kroenke
Mpaka sasa bado haijajulikana kama Mzee Wenger ataongeza mkataba ama laa baada ya kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 21.
Masharti ya mkataba mpya yalikubaliwa miezi kadhaa iliyopita, lakini hakuna kilichofanyiwa kazi mpaka hivi sasa.
Mipango ya Mzee huyo ilikuwa kuendelea kubaki katika klabu hiyo lakini hali ilibadilika katika kipindi cha hivi karibuni baada ya kupingwa vikali na baadhi ya mashabiki wakihitaji kocha huyo kuachia ngazi.
Mashabiki wa klabu ya Arsenal wakibeba mabango yanayo onyesha kumpinga kocha Arsenal Wenger
Hali kidogo imekua shwari baada ya kuifunga Chelsea 2-1 katika fainali za kombe la FA siku ya Jumamosi na kumfanya Wenger kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye kombe hilo huku Arsenal nayo ikiwa na mafanikio zaidi kuchukua kombe hilo.
No comments