Baada ya Msiba wa Mkewe......Mwakyembe Leo Kaongea na Waandishi wa Habari
Leo Jumatano ya July 26 ikiwa ni siku 11 zimepita toka utokee msimba wa mke wa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe, leo ameongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam.
Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan.
Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.
No comments