Kagame Ajitabiria Ushindi Kishindo Rwanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame tayari anadai kuwa mshindi katika uchaguzi ujao wa Rais utakaofanyika tarahe nne mwezi ujao.
Kagame amewaambia wafuasi wake katika mkutano wa kwanza wa kuanza rasmi kwa kampeni nchini humo kuwa matokeo ya uchaguzi tayari yalijulikana mnamo mwaka 2015 wakati Wanyarwanda waliposhiriki katika kura ya maoni ili bunge kuifanyia katiba mageuzi ya kumruhusu kugombea muhula mwingine.
Kagame amesema wapinzani wake hawawezi kubadilisha mapenzi ya wananchi kuwa yeye ndiye chaguo lao.
Paul Kagame licha ya kuwa anasifiwa kwa kuleta uthabiti katika taifa hilo la takriban watu milioni 12, anashutumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia mkono wa chuma kuliongoza taifa na kuwakandamiza wapinzani.
No comments