Mazoea na mashabiki sitaki – Linex
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Linex amekataa mashabiki zake kumzoea kuwa anafanya muziki wa aina gani.
Akiongea katika Planet Bongo ya EA Radio msanii huyo amefunguka kuwa ana uwezo wa kuimba aina yoyote ya muziki hivyo hataki mashabiki zake kumkariri kuwa anafanya muziki wa aina gani.
“Sitaki mashabiki wazoe kuwa nafanya muziki wa aina moja, nina uwezo wa kuimba, kurap kama Edo Boy ndio maana kwenye ngoma yangu nimeimba na kurap,” amesema Linex.
Linex ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu amerudi upya katika muziki akiwa na ngoma yake ya ‘Got me’ aliyiomba kwa maadhi ya kijamaika. Pia msanii huyo ambaye ni baba wa mtoto mmoja wa kiume Jaheim, amekanusha madai ya kutumia kilevi.
No comments