Mkuu wa TEHAMA wa tume ya uchaguzi nchini Kenya akutwa amefariki
Mkuu wa kitengo cha TEHAMA wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, ambaye alitoweka siku ya Ijumaa amepatikana akiwa amefariki.
Polisi wamesema kuwa mwili wa afisa huyo aliyetambulika kwa jina la Chris Musando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la kikuyu lililo vitongoji vya jiji la Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Bwana Musando alikuwa akihusika na usambazaji wa vifaa vyaa eletroniki ambavyo vingetumiwa kutambua wapiga kura na kwa upeperushaji wa matokeo wakati wa uchaguzi mkuu wiki ijayo.
No comments