Usikose Hizi Hapa

Ni Zambia na Zimbabwe Fainali ya COSAFA

Michuano ya COSAFA Castle Cup inayoendelea huko nchini Afrika Kusini imefikia patamu mara baada ya hapo jana kushuhudia baadhi ya timu zikitinga hatua ya Fainali ya michuano hiyo.

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  ikicheza na Zambia mchezo wa Nusu Fainali ya CODAFA
Timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) imekuwa ya kwanza kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Taifa Stars kwa jumla ya magoli 4-2 katika hatua ya Nusu Fainali mchezo ulichezwa katika dimba la Moruleng nchini Afrika Kusini.
Katika mchezo huo beki wa Stars, Erasto Nyoni alianza kuipatia Taifa Stars bao la kuongoza katika dakika ya 14, lakini katika dakika ya 44 Brian Mwila, akaisawazishia goli hilo ’Chipolopolo’ dakika moja baadae Justin Shonga akaifungia Zambia goli la pili.
Wakati wa kipindi cha Pili, dakika ya 56 Chipolopolo wakaongeza goli la tatu kupita kwa Chirwa aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Justin Shonga akahitimisha karamu ya magoli wakati Simon Msuva akiishindia Stars gold la pili mchezo uliomalizika kwa idadi hiyo ya magoli na Zambia kutinga Fainali.
Wakati Zimbabwe imetinga hatua ya Fainali baada ya kuifunga timu ya taifa ya Lesotho kwa jumla ya magoli 4-3 kwa matokeo hayo inaifanya Zimbabwe kucheza na Zambia katika mchezo wa fainali utakao chezwa siku ya Jumapili ya Julai 9.
Mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo ya COSAFA Castle Cup utazikutanisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Lesotho siku ya Ijumaa.
Wachezaji wa Timu ya timu ya taifa ya Zambia na Zimbabwe 
Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itaingia katika mchezo huo wa kutafuta mshindi watatu wa michuano hiyo mikubwa huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 1-1 na Lesotho Juni 10 mwaka huu Katinka mchezo wa kwanza wa kundi ‘ L ‘ kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa mwaka 2019 nchini Cameroon na hivyo mchezo huo unamaana kubwa kwa timu zote mbili.

No comments