Rais Magufuli atangaza kiama kwa waliojenga barabarani
Rais John Magufuli amesema kwamba waliojenga nyumba kwenye hifadhi za barabara na reli wajiandae kisaikolojia kwani ni lazima waondoke.
Rais amesema Wananchi wa Kaliua wanahitaji maendeleo hivyo ikiwa nyumba zipo kwenye hifadhi ya barabara au reli zibomolewe haraka ili kuleta maendeleo ya nchi.
Alisema kwamba kuna sheria hivyo lazima zisimamiwe na lazima zifuatwe, sheria ni msumeno lazima tuzifuate.
Alisema hayo wakati akizindua barabara ya Kaliua hadi Kazilambwa akidai kwamba hawajaomba msaada kwa mtu yeyote fedha za ujenzi wa barabara hizo.
Alisema hakuna wizara ngumu kama Wizara ya Ujenzi kwa sababu yeye mwenyewe aliwahi kuwa waziri katika wizara hiyo.
“Msione vyaelea vimeundwa na waundaji ndiyo sisi, kazi ya barabara imeisha, jukumu lililobaki ni kuitunza."
No comments