Tafiti: Tanzania kubakiwa na hifadhi mbili pekee kati ya 16
Mabadiliko ya tabia nchi yameathiri kwa kiasi kikubwa sekta za mbalimbali na kupeleka baadhi ya sehemu kuwa na uhaba wa mvua na pia ongezeko la joto kwenye eneo la Antarctic limepekea kuyeyuka kwa barafu na kuleta athari.
Mkurugenzi wa Kituo cha Sayansi Tembo, Dk Alfread Kikoti ametoa tahadhari kuwa ifikapo mwaka 2050 Tanzania itabakiwa na hifadhi mbili peeke kati ya 16, hifadhi hizo ni Ruaha na Selou. Iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa basi janga hilo itaikumba nchi hii.
Utafiti unaonyesha Ruaha na Selou zitabaki kutokana na sababu ya hali ya kijiografia pamoja na ikolojia. Kwa mujibu wa mtaalamu huyo mabadiliko ya tabia ya nchi yataleta athari kwenye hifadhi zingine ikiwamo ukame utakaotokana na kukauka kwa maji na malisho ya wanyamapori.
Dk Kikoti alizungumza kwenye mkutano wa wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari uliofunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ambaye aliwaomba kuweka mbele uzalendo wakati wa kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Kwa upande wa Alain Kijazi , Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), ameelza kuwa vyombo vya habari vimechangia kutangaza vivutio na kwa wageni kutoka nchi za nje ili kuvitembelea.
Nao wahariri waliohudhuria mkutano huo walionyesha hofu yao juu ya taarifa ya hatari ya kutoweka kwa hifadhi na kuahidi kutumia nafasi zao kuielimisha jamii
No comments