Ubovu wa maproducer unanifanya nishindwe kutoa hit – PNC
Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, PNC amefunguka kuwa kipindi hiki waandaaji wa muziki sio wabunifu kama zamani ndiyo maana anapata tabu kutengeneza ngoma kali kwasasa.
Msanii wa Bongo Fleva PNC (picha kutoka Bongo5)
PNC ametolea mfano wa ngoma yake ya ‘Mbona’ ambayo alimshirikisha Mr Blue amesema muandaaji wa wimbo huo alitumia ubunifu sana kwani yeye aliimba taratibu ila vinanda na midundo iliyopangiliwa ndiyo ilinogesha wimbo huo mpaka ukawa ngoma kubwa kwa kipindi kile.
“Mimi nadhani kwa sasa nashindwa kutoa hit kali kama zamani kutokana na kupungua kwa ubunifu wa maproducer utakuta siku hizi hawatumii nguvu nyingi kama zamani”,amesema PNC kwenye mahojiano yake na Bongo5 huku akitolea mfano wa ngoma yake iliyofanya vizuri miaka ya nyuma ya Mbona.
“Nakumbuka kipindi kile narekodi ngoma yangu ya ‘Mbona’ niliingiza sauti kawaida sana kwa MJ kipindi kile Producer alikuwa Bizman lakini aliingiza vinanda na midundo kwa ubunifu ngoma ikawa kali mpaka leo nikiisikiliza naona kama sio mimi niliyeingiza vocal”,amesema PNC .
Kwa sasa PNC amerudi kwa kasi kujaribu gemu kwa kuachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Nyota’ ambao mdundo umetengenezwa Mazuu Records na video imeongozwa Pizzo Mtema.
No comments