USAJILI: Liverpool yasajili beki kisiki wa Hull City
Miamba ya soka barani Ulaya imeendelea kutafuta wachezaji wa kuwasajili katika timu zao kwa ajili ya msimu ujao. Liverpool ya Uingereza nayo imeendelea kukijenga kikosi chao kwa kumsajili beki wa kushoto Andy Robertson.
Mchezaji huyo ana umri wa miaka 23 na ni raia wa Scotland, amesajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 10 akitokea Hull City ya Uingereza kwa mkataba wa maiak mitano.
Mchezaji huyo ana umri wa miaka 23 na ni raia wa Scotland, amesajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 10 akitokea Hull City ya Uingereza kwa mkataba wa maiak mitano.
Robertson amefanikiwa kuichezea Hull City kwa misimu mitatu huku akiichezea mechi takribani 99 na kufunga magoli matatu.
Mchezaji huyo anakuwa watatu kusajiliwa na Liverpool katika msimu huu wa usajili baada ya Mohamed Salah kutoka AS Roma na Dominic Solanke aliyetokea Chelsea.
No comments