Usikose Hizi Hapa

Video: Rama Dee akubali mastaa Bongo kutoka na wapenzi waliowazidi umri

Mkali wa Muziki wa RnB Bongo, Rama Dee amesema haoni tatizo kwa mastaa kutoka kimapenzi na watu waliowazidi umri ilimradi muhusika ana miaka 26 na zaidi.



Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Nibebe’, ameiambia Bongo5 kuwa ikiwa wanaoamua kufanya hivyo wanapendana hamna shida.
“Mimi nafikiri kwenye mahusiano hayachagui umri kwa sababu ukisema huyu jamaa mbona mdogo amempenda huyu mama mkubwa au huyu mzee amependana na huyu dada mdogo labda yuko chini ya miaka 20 au 25 unaweza kusema hapo sawa,” amesema Rama Dee na kuongeza.
“Lakini kama mtu amefikia miaka 26 na kuendelea juu, mimi naona ni sawa kwa sababu hata wazee wanapenda pia, hata Mmama anapenda pia,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine Rama Dee ameeleza sababu ya ukimya wake baada ya kuachia ngoma ya Kipenda Roho, “nilikuwa nafanya mambo mengi sana na sehemu ambayo ninaishi kuna shughuli nilikuwa nazifanya na hapa pia Bongo kuna vitu vingi navifanya.
“Mimi vile vile ni mkulima, najaribu kutega sehemu nyingi ilimradi nisije kuaibika hapa mjini, kwa hiyo mambo yanakuwa mengi hadi wakati mwingine nakuta nashindwa kujigawa lakini huwa napanga nikishamaliza vitu vyangu niwe nakaa chini nifanye muziki,” amemaliza kwa kusema.

No comments