Shilole akana kukwapua mume wa mtu
Msanii wa mziki Bongo, Shilole amekatana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mume wa mtu.
Hayo yamebuika mara baada ya muimbaji huyo kutangaza kuolewa ndani ya mwaka huu na mipango yote ya ndoa kukamilika kama kutolewa mahari.
“Siyo kweli sijanyangamya mume wa mtu, huyo bwana alikuwa naye lakini waliachana, before hata yangu, kwa hiyo haya mambo yanatokea kwa sisi haswa watu wa mashughuli mjini, huyo dada kusikia nipo na huyu kaka leo itakuwa inamchoma, hapo ndipo panaanzia utata,” Shilole amekiambia kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha Times Fm.
Hata hivyo amesema kuwa suala hilo halimuumizi kwa sababu ukweli anaujua, huku akiongeza mume wake mtarajiwa amekubali kazi yake anayofanya (muziki).
“Ndiyo amekubali kwa sababu amenikuta kwenye muziki na ndio kazi yangu na ameanza kunijua kupitia muziki wangu, kwa hiyo lazima anisapoti na anapenda kazi yangu,” amesisitiza.
No comments