Hali baada ya Kenyatta kutangazwa mshindi Kenya
Hali ya kawaida imeanza kurejea mjini Garissa siku moja baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais kutangazwa.
Rais Kenyatta alitangazwa mshindi wa urais Ijumaa usiku baada ya kupata kura 8, 203, 290 sawa na asilimia 54.2 zilizopigwa.
Mgombea wa upinzani Raila Odinga alipata kura 6,762,224 sawa na asilimia 44.7
Baada ya matangazo, visa vya maandamano viliripotiwa katika baadhi ya maeneo ambayo ni ngome ya upinzani, mfano Kisumu, Homa Bay na Migori magharibi mwa nchi hiyo.
Sehemu ya soko kuu mjini humo iliteketezwa Jumatano wakati wa ghasia kati ya wafuasi wa wagombea wawili wa ugavana. Lakini jana na leo hali imekuwa tulivu.
Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay, amepiga picha hizi za wananchi wakiendelea na shughuli zao za kawaida leo asubuhi.
No comments