Jaguar ashinda kiti cha ubunge
Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Jaguar amefanikiwa kuibuka mshindi katika kinyanganyiro cha nafasi ya ubunge katika jimbo la Starehe lililopo Nairobi nchini humo kwa kuwapiku wapinzani wake Steve Ndwiga na Boniface Mwangi.
Kupitia mtandao wa Instagram Jaguar ameandika “Nothing would count without God Above. I thank the People of Starehe for having the confidence and trust in me to represent them in Parliament. I thank all my supporters, friends and family who stayed out late campaigning. I also congratulate my Worthy Opponents; Steve Mbogo, Boniface Mwangi and Hon Kwenya who put up well spirited campaigns. This is not only a win for Starehe but a win for all the youth in Kenya who look towards a more promising future for Kenya. Let’s now build the Starehe that we all want. God bless you all.”
Jaguar atakuwa msanii wa kwanza Kenya kuwa mbunge ambapo anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao ni wabunge Afrika Mashariki ambapo kuna Joseph Haule ‘Professor Jay’ mbunge wa Mikumi, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na Robert Kyagulanyi Ssentamu ‘Bobi Wine’ mbunge wa Kyadondo Mashariki mwa Uganda.
No comments