Mhe. Ngonyani (Majimarefu) aomba Rais Magufuli aongoze miaka 20
Mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani (Profesa Maji Marefu) amesema kuwa anaomba Rais Magufuli aongoze miaka mingine 10 ya kuongoza ili atawale nchi hii kwa miaka 20 nchini Tanzania.
Prof. Ngonyani amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa standi mpya ya mabasi iliyopo katika halmashauri ya mji wa Korogwe ambapo amedai kuwa Rais Magufuli anafanya kazi ambayo Watanzania wanaipenda na inaonekana hivyo itakuwa ni jambo jema kama ataongezewa muda zaidi ya kuongoza.
“Mhe. Rais wewe ni jembe na unakumbuka ukiwa waziri wa barabara, ujenzi nilikufuata kule ofisini kwako nikakuomba barabara ya kutoka segera kwenda mpaka
Same niwekee lami na ukaniambia mwanangu nenda na ukaniambia na hiyo kazi wiki ijayo inaanza na ukaifanya kazi hii na siku uliyomleta Muheshimiwa Rais ukatupandisha pale na ukatusifia sana basi mimi bahati nzuri wewe umeletwa na Mungu na katika watu watakao sema katika Halmashauri kuu ya Taifa mimi ni mjumbe. Wewe uongezewe miaka hii miaka 10 haitutoshi uongezewe miaka ufanye kazi miaka 20,” alisema Ngonyani.

“Na hilo pendekezo la ilani ya uchaguzi lije mapema Mashekh wapo hapa, viongozi wa dini wapo hapa na sisi waganga wa kienyeji tupo hapa tutakuombea hilo wazo litapita.Mtu anayefanya kazi hakuna kumbadilisha badilisha, unafanya kazi ambayo watu wa Tanzania wanaipenda sasa tukibadilisha badilisha matokeo yake tunaweza kupata mtu ambaye ataimaliza nchi yetu niliona niliseme hili Mheshimiwa.”
No comments