Sijawahi date na star na sitaki – Dayna Nyange
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hajawahi kutoka kimapenzi na star yeyote Bongo na hataki kufanya hivyo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovya’, amesema sababu ya maamuzi yake ni kufanya mahusiano yake kuwa binafsi zaidi.
“No siyo star, sijawahi date na star na sitamani ku-date na star na sitaki ku-date na star na sito-date na star,” Dayna ameiambia Bongo5.
Pia msani huyo ameeleza kuwa yupo kwenye mahusiano lakini anapenda kuyafanya siri sana kiasi kwamba hata mama yake mzazi hajui.
“Naogopa atakasirika ataniacha kwa sababu nampenda, ni mtu ambaye ana wivu, nilishawahi kusema sina mahusiano akachukia nikaoni ok, isiwe shida nipo kwenye mahusiano lakini hayatambuliki kokote hata mama hamjui,” amesema Dayna.
No comments